Blog Post

HOJA : HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUPANDISHWA HADHI KUWA HOSPITALI YA TAIFA


Na Selemani Wambura 

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ameunga mkono hoja ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa (BMH) kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya taifa, akiahidi kuisukuma ajenda hiyo 

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya hospitali hiyo, Mchengerwa amesema ataendelea kulikumbusha suala hilo kwa Rais Samia Suluhu Hassan kila atakapopata fursa. ngazi za juu za maamuzi.

Amesema BMH imekua kwa kasi na kuwa mfano wa utoaji wa huduma bora za afya, ikihudumia wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini .

Kwa mujibu wa waziri huyo, kupandishwa hadhi kwa hospitali hiyo kutakwenda sambamba na maboresho ya kimfumo, yakiwemo kuongeza watumishi, kuimarisha miundombinu, kuboresha vifaa tiba na kuanzisha huduma mpya za kisasa. kwa viwango 

Ameeleza kuwa serikali inalenga kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha huduma za kibingwa na bingwa bobezi, sambamba na maono ya Julius Nyerere. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, Edward Hoseah, ameomba serikali kusaidia kutatua changamoto za hospitali hiyo, ikiwemo upungufu wa watumishi, magari ya huduma na deni la zaidi ya shilingi bilioni 14.39.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Abel Makubi, amesema katika kipindi cha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, hospitali hiyo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu