Na Mwandishi wetu 


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewashukuru wadau na wananchi kwa kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kipindi cha mwaka 2025.


Ushirikiano huo ulikuwa nguzo muhimu ya mafanikio katika utoaji wa huduma za kisheria nchini.


Kupitia imani na mshikamano huo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kutoa huduma bora za Ushauri wa Kisheria, Upekuzi wa Mikataba pamoja na Uandishi wa Sheria, hatua iliyochangia kuimarika kwa mifumo ya kisheria na utendaji wa taasisi mbalimbali za umma.


Hata hivyo, Ofisi hiyo imeeleza kuwa mafanikio hayo yasingewezekana bila ushiriki wa karibu wa wananchi na wadau wake.


Ikianza mwaka mpya wa 2026, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeahidi kuendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi wa hali ya juu, ikiwakaribisha wadau wote kuendelea kushirikiana katika kujenga mwaka mpya uliojaa mafanikio zaidi kwa maendeleo ya taifa.

                 https://www.instagram.com/p/DTDu_8wADPN/?igsh=Nnd6eXFlYjV0MzV2