Blog Post

WAZIRI KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WA NMB NA KUWAOMBA KUWEZESHA VIJANA







Na Omary Mbaraka 

Waziri wa kazi ajira na vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete Leo alitembelewa na ugeni wa Watendaji wa Benki ya NMB wakiongozwa na Bi. Vicky Bishubo, Meneja mahusiano Benki na Serikali waliokuja kujitambulisha na kutambulisha bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo. 

Katika kikao hicho Mhe Kikwete aliiwakaribisha ofisini kwake na kuwatambulisha baadhi ya maeneo ambayo benki hiyo inaweza shirikiana na Serikali katika kufanikisha uwezeshaji wa Vijana na Jamii.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu