Blog Post

DANGOTE WAPATA NASAHA BAADA KUMTEMBELEA WAZIRI KIKWETE






Na Omary Mbaraka 


Leo tarehe 8 may 2025 Ujumbe wa Kiwanda cha Kutengeneza Cement Cha Dongote ulimtembelea waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete ofisini kwake jijini Dodoma wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda hicho Nchini Bwana Adeyemi Fajobi. 

Katika mazungumzo yao walijikita zaidi kuzungumzia maeneo yenye changamoto na utatuzi wake. Pia Mhe Kikwete aliwakumbusha umuhimu wa kiwanda hicho kwa Watanzania haswa Ajira na kukuza uchumi wa miji yetu ikianza na Mkoa wa Mtwara. Kwa upande wake Bwana Adeyemi amemsisitizia Waziri kuendelea kufanya kazi kutatua changamoto zinazotokana na mahala pa kazi na kuiomba serikali kuendelea kushirikiana nao. Mh. Waziri alimuahidi kuwa serikali itaendelea kufanya kazi nao

Post a Comment

0 Comments

Close Menu