Blog Post

KIKWETE ASHIRIKI UZINDUZI MAONYESHO YA SABA SABA DAR

 









Na Omary Mbaraka 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete ameshiriki Uzinduzi wa Maonyesho ya 49 ya Wakulima maarufu 77 yaliyozinduliwa katika Viwanja vya 77 , Barabara ya Kilwa , Dar Es Salaam. 

Katika maonyesho hayo, ambayo yalizinduliwq na Rais Mwinyi yamewakutanisha wadau mbalimbali wanaofanya biashara ndani na nje ya Nchi ikiwemo nchi za China, India, malaysia na nchi nyengine za Ulaya, Afrika na Asia.Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa mabanda ya maonyesho, Rais  Mwinyi ambaye pia alipata nafasi ya kutembelea banda la Waziri ambapo Aliona kazi mbalimbali zinazofanywa ikiwemo kupitishwa katika mifumo ya Tehama iliyoundwa na vijana wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia kutambua athari za hali ya hewa zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na hali joto na pia mfumo maalum wa kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto ikiwa ni sehemu mkakati wa kupambana na majanga.

Akiwa Katika banda la ofisi ya Waziri Mkuu, Rais Mwinyi akiwa na Mwenyeji wake Waziri Kikwete, alipata nafasi ya kutembelea shughuli mbalimbali na mwisho kuona ikiwemo matunda ya uwekezaji ikiwemo sukari inayozalishwa katika kiwanda cha Mkulazi ambacho ni Kiwanda kilichotengenezwa kwa Ubia kati ya Taasisi ya NSSF na kampuni Tanzu ya SHUMA inayomilikiwa na Jeshi la Magereza.

Rais Mwinyi alimaliza Ziara hiyo kwa kutoa zawadi kwa washiriki, Wadhamini na washindi katika vitengo mbalimbali vya uzalishaji mali.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu