Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete Jana katika tuzo ya uandishi bora iliojulikana SAMIA KALAMU AWARDS Pia alimkabidhi zawadi nono Mwandishi wa habari aliyeshinda katika uandishi bora sekta ya vijana na amesema wizara imejipanga kuinua vijanaI.
Wizara yampa milioni 5, Cheti, Laptop na ziara za Wizara kutembea nae ili kuleta mageuzi chanya kwa Vijana alisema Mhe Kikwete
Jana Jumatatu kwenye Ukumbi wa Super Dome Jijini Dar es Salaam palifanyika tuzo za Samia Kalamu Awards ili kuwatambua Waandishi walioandika makala zinazoleta mageuzi chanya kwenye Jamii kwenye sekta mbalimbali. Mgeni rasmi alikua Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwenye Sekta ya Vijana, mshindi alikua Bw. Gilfred Msengezi wa Azam Media aliyeshinda kupitia Kazi yake ya *VIJANA WANAVYOBADILI NYWELE ZA BINADAMU KUWA MBOLEA YA MAZAO.* Hivyo basi Mhe Kikwete alimkabidhi zawadi nono mshindi huyo kama njia ya kutambua mchango wake katika kuleta mageuzi yenye tija kwa Vijana.
Waziri Kikwete kwa niaba ya Wizara mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan alimkabidhi mshindi huyo cheti cha utambuzi, laptop ya kisasa kwa ajili ya kurahisisha kazi zake za uandishi, kiasi cha fedha milioni 5 pamoja na kumjumuisha kwenye kazi zote za Wizara ili aendelee kuleta mabadiliko chanya kwa Vijana.
Nae Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe DKT Samia Suluhu Hassan alizishukuru taasisi za TAMWA na TCRA kwa kuandaa tuzo Hilo ambalo alisema litachochea uandishi bora hapa nchini huku akiwaasa waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa Taifa lao ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuvutia wawekezaji toka nje kuja kuwekeza hapa nchini.
0 Comments