Blog Post

SERIKALI KUWAWEZESHA WENYE ULEMAVU KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII-WAZIRI KIKWETE

 






Na Omary Mbaraka 

Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete ameshiriki kongamano la Wenye Ulemavu lililoandaliwa na Ikupa Trust Fund, lililofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar, Dodoma Juni 09,2025.

 Kupitia kongamano hilo amewahakikishia Washiriki utayari wa serikali kushirikiana nao katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kushiriki shughuli zote za kijamii ikiwemo kujenga uchumi na kujenga Jamii itakayopambana kwa ajili ya maslahi mapana ya Wenye Ulemavu.

Katika hatua nyingine Mhe Kikwete amekabidhi vifaa wezeshi kwa wenye Ulemavu vikiwemo Fimbo Nyeupe,  Mafuta ya Saratani ya Ngozi chupa 103 kwa Wenye Ualibino, Magongo kwa wenye Ulemavu wa miguu, Kofia pana na Miwani kwa wenye Ualbino.

Mhe Kikwete akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, amewakumbusha  Watu wenye Ulemavu kuwa nao ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa, hivyo wanapaswa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo, sawa na wasio na ulemavu jambo ambalo ndio dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu