Na Omary Mbaraka
Tarehe 2 April 2025 Waziri katika ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana ajira na wenye ulemavu pia mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhwani Jaksya Kikwete alipata nafasi ya kutoa maelezo ya shughuli ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kibaha Mkoa wa Pwani,
Akizungumza mbele ya Wananchi waliojitokeza na Viongozi wa Kitaifa wakiongozwa na Aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Shughuli hiyo Dr. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefuatana na Viongozi mbalimbali akiwemo Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. Dotto Biteko , Naibu Waziri Mkuu Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Waziri Wa Nishati na Alhaj Hamza Juma ,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Pili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliwakumbusha Watanzania Umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao unatokana na Ujumbe unaosambaza. Pia kuwakumbusha Ujumbe wa Mwenge Mwaka huu ambao ni *Jitokeze Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu* huku zile jumbe nyengine ikiwemo ya mapambano dhidi ya Rushwa, maradhi kama VVU/Ukimwi, Malaria, Lishe zikiwa bado zinaendelea.
Dr. Philip Isdor Mpango, mgeni rasmi alitumia nafasi hiyo kuwahimiza viongozi na wanaosimamia shughuli za uchaguzi kuhakikisha haki inatolewa na kuondoa hali za kuchafua amani. Mwisho aliwasha mwenge wa Uhuru na kuukabidhi Mkoa wa Pwani ambapo Mkuu wa Mkoa Alhaj Aboubakar Kunenge alikuwa kiapo cha kuukimbiza mwenge kwenye halmashauri 9 za Mkoa wa Pwani.
Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru zilizowashwa Kibaha, Pwani zinatarajiwa kuhitimishwa Mkoani Mbeya tarehe 14 Oktoba 2025 baada ya kutembea, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri 195, katika Mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments