Na Omary Mbaraka
Namibia Yasitisha Kuingia Bila Visa kwa Raia wa Marekani katika Hatua ya Kijasiri ya Kidiplomasia Ili Kuzuia Uchukuaji wa Madini Yake Kinyume cha Sheria.
Kuanzia leo, Aprili 1, Serikali ya Namibia itahitaji kila raia wa Marekani anayeingia nchini humo kuwa na Visa. Mtu yeyote kutoka Marekani atakayekamatwa akiwa Namibia bila Visa itakayotolewa rasmi atatangazwa kuwa “MGENI HARAMU” na atatendewa kwa njia sawa kabisa na jinsi Donald Trump anavyowatendea wahamiaji wa Kiafrika nchini Marekani.
Baada ya tangazo hili kutolewa, zaidi ya raia 500 wa Marekani waliokuwa wakichimba Almasi, Dhahabu, Urani, Shaba, na madini mengine nchini Namibia bila Visa waliwasilisha maombi ya Visa ili waendelee na uchimbaji wao, lakini wote walikataliwa na wameamriwa kuondoka nchini leo (Aprili 1) au wafukuzwe kwa nguvu kuanzia kesho.
Namibia ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa Almasi duniani, na sasa chini ya Utawala mpya wa Rais Natumbo Nandi Ndaitwah wanataka kuchukua udhibiti kamili wa migodi yao ya Almasi. 🇳🇦👏
0 Comments