Blog Post

JENGO LA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA YA TANZANIA LAZINDULIWA NA RAIS SAMIA

\


Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuongeza bajeti ya Mahakama kutoka Shilingi bilioni 160 hadi bilioni 321 ili kuboresha ufanisi wa Mahakama nchini. Akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama, na Makazi ya Majaji Jijini Dodoma, Rais Samia alisisitiza kuwa Serikali inatilia mkazo kuongeza ufanisi katika sekta ya Mahakama.

Katika hotuba yake, Rais Mhe Dkt  Samia alisema, "Serikali katika hatua ya kufanya Mahakama iende kwa haraka tumeongeza bajeti ya Mahakama kutoka Tsh. bilioni 160 mwaka 2021 na mwaka huu wa fedha tuko kwenye Tsh. bilioni 321. Niwaahidi kuwa Serikali kwa pande wetu tutajitahidi kutenga fedha hizi na kuzitoa kwa wakati."alisema Mhe SAMIA.

Aidha, Rais Samia alieleza kuwa, katika miaka minne ya utawala wake, hajawahi kuzuia safari za Majaji kwani anaziona kuwa ni sehemu muhimu ya mafunzo na kuongeza ufanisi kwa Mahakama. Alisisitiza kwamba Majaji wanaposhiriki mikutano na safari za kimataifa, wanapata ujuzi na uzoefu unaowafaidi wanapo

Post a Comment

0 Comments

Close Menu