Blog Post

DKT SAMIA AUKARIBISHA UGENI MKUBWA DAR ES SALAAM

 
Dkt. Samia Suluhu Hassan, 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 


Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania,  amewakaribisha wageni mbalimbali watakaoshiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati kuanzia kesho Jumatatu, Januari 27-28, 2025.

Mkutano huo utakaofanyikia ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JINC) jijini Dar es Salaam utawakutanisha zaidi ya marais 25 na  mawaziri wakuu na mawaziri wa fedha na nishati 60 wa Afrika.

Kupitia  kipande cha video, Rais Samia amewakaribisha wageni hao kushiriki mkutano huo utakaoangazia masuala ya nishati safi na mwisho wa mkutano mapendekezo yatatolewa na kwenda kufanyiwa kazi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.

 lMwandishi WA habari hizi amezungumza na wanazuoni wa masuala ya uchumi wameangazia fursa mbalimbali ambazo Watanzania watanufaika kutokana na ugeni huo mkubwa.

Pia barabara zipatazo tisa kufungwa jijini Dar es salaam ikiwemo barabara kutoka uwanja wa ndege kwenda mjini na watumishi kushauriws kufanya kazi nyumbani kwa siku mbili


Post a Comment

0 Comments

Close Menu