Blog Post

MHE KOMBO ASHIRIKI SHEREHE ZA MIAKA 107 YA UHURU WA FINLAND

 Na Omary Mbaraka 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) ameshiriki sherehe ya Maadhimisho ya miaka 107 ya Uhuru wa Taifa hilo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Finland hapa nchini.


Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo Waziri Kombo aliyealikwa kama Mgeni Rasmi licha ya kuipongeza Serikali ya Finland kwa kuendelea kulinda Uhuru wake na kudumisha amani na usalama pia, amepongeza hatua ya maendeleo ya kiuchumi iliyofikiwa na Taifa hilo.


Aidha, Mheshimiwa Waziri aliongeza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kukuza mahusiano ya kidiplomasia yaliyodumu kwa muda mrefu baina ya mataifa haya mawili kwa manufaa ya watu wake.


Kwa upande wake Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Theresa Zitting amesema Serikali ya Finland itaendelea kutumia matunda ya Uhuru wake kukuza mahusiano mazuri ya Kidiplomasia yaliyopo baina yake na Mataifa mengine ulimwenguni.  


Sherehe za Maadhimisho hayo ambazo zimefanyika katika Makazi ya Balozi wa Finland Masaki jijini Dar es Salaam zimehudhuriwa na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.


Finland ilipata Uhuru wake Disemba 6, 1917

Post a Comment

0 Comments

Close Menu