Na Omary Mbaraka
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi DKT Moses Kusiluka na Kutangazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Sharifa B Nyanga leo, Raisi DKT Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kadhaa ya viongozi ikiwemo kumteua Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mhe. Profesa Kabudi ataapishwa pamoja na viongozi wengine wateule tarehe 10 Desemba 2024 Zanzibar.Ifuatayo ni taarifa rasmi kutoka kwa msemaji wa Rais Sharifa Nyanga
0 Comments