Blog Post

KAMPUNI M & M PACKAGE YAPUKUTISHA VIDOLE VYA MFANYAKAZI WAKE


Na Ismail Mangola

Kampuni ya M&M PACKAGE LTD iliyopo eneo la Majohe Ilala jijini Dar es Salaam,  imeingia matatani baada ya mfanyakazi wake aliyetambulika kwa jina la Joseph Amos  kupukutika vidole vinne vya mkono wa kulia akiwa kazini (Machine Operator).

Baada ya kupata malalamiko toka kwa muathirika, chombo hiki kilifika na kuonana naye ambapo alikiri kutokewa na ajali hiyo na kuonyesha mkono huo ambao umeonekana una ulemavu wa kudumu.

Hata hivyo kijana Joseph alishukuru kukimbizwa katika hospitali ya KIBONG'OTO iliyopo Gongolamboto mnamo 9 February 2024 majira ya sàa 6 usiku.

"nilikuwa kazini usiku wa tarehe 9 February mwaka huu majira ya sàa sita usiku, mashine ilinikata vidole vyangu vinne nikaanguka na kupoteza fahamu, kwani nilikuwa Sina hata vitendea kazi vya kujikingia na ajali". Joseph alisema.




Chombo hiki hakikuishia hapo, kwani kilimtafuta Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo ambapo kilimpata mmoja wa wakurugenzi ambaye alijitambulisha kwa jina la Mussa Abdallah ambapo alikiri kwa kusema yeye ndiye mwenye KIWANDA na tukio Hilo analifahamu.

"tatizo la kijana Joseph nalifahamu, na nilimsaidia ipaswavyo nilimpeleka hospitali na naendelea kumpatia huduma Hadi Hivi sasa". Alisema Mussa.

Hata hivyo chombo hiki bado kinakamilisha uchunguzi wake Ikiwemo kwanini walikwepa kuripoti Polisi na kuchukua PF3, haki za muathirika, mkataba wake wa kazi pamoja na Wizara husika kupitia kwa Waziri wake, na kwanini muathirika aliingizwa uanachama WCF baada ya kuumia? Na kwanini hakuna huduma ya kwanza (First AID) kwenye Kampuni nk

Post a Comment

0 Comments

Close Menu