NA OMAR MBARAK
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali inaendelea kupambana kutatua changamoto zinazowakabili vijana.
Ridhiwani ameyasema hayo alipokuwa akifunga Kongongamano la Kitaifa la Agenda ya Amani na Usalama kwa Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Akifunga kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Mhe Ridhiwan amewaasa vijana kuwa mabalozi wa amani na usalama na kushiriki ulinzi wa nchi yao.
Alikumbusha kuwa hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali yao ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana ikiwemo ukosefu wa kazi, athari za matumizi mabaya ya Teknolojia /Mitandao katika kupashana taarifa muhimu zinazowahusu vijana, Uundwaji wa Baraza la Vijana, Uwezeshwaji.
0 Comments