Blog Post

MOJA YA NGUZO ZA MAFANIKIO NI UPENDO-KIKWETE

 NNa Omar Mbaraka



Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaongea na Viongozi wa Chama  cha CCM na wa Halmashauri ya Chalinze alipowaalika kwenye Futari nyumbani kwake Msoga. 

Futari hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama wilayani hapo akiwepo Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndg. Abdul sharif Zahor na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya kutoka kata zote za Jimbo la Chalinze ililenga kuwakutanisha viongozi wa wilaya ikiwa na malengo ya kuupokea mfungo wa mwezi wa Ramadhani, kuwaombea na kuwarehemu viongozi waliowahi kuongoza Wilaya hiyo na amani ya Wilaya hiyo na Wazee.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu