Na Omar Mbaraka
Wakati huohuo naibu Waziri Kikwete Achangia Gharama za Matibabu za Majeruhi wote.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wamewatembelea majeruhi wa ajali ya Gari zilizogongana juzi tarehe 29 Machi 2024. Ajali hiyo ya gari ya Abiria aina ya Coaster iliyokuwa imebeba washabiki wa timu ya Simba waliokuwa wanasafiri toka Mbeya kuelekea Dar Es Salaam kuangalia mpira na hivyo kugongwa na lori la mizigo likiingia barabarani kutoka kupima Uzito kwenye Mzani maeneo ya Vigwaza.
Akiongea kabla ya kumkaribisha Spika Mhe kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze alitoa pole kwa uongozi wa Simba na wafiwa na kuwaombea kwa Mungu warudi salama Mbeya.
Na Katika tukio la Kiungwana Mhe Kikwete aliamua kulipa gharama za huduma za wote waliohudumiwa hospitalini hapo Msoga jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 3.8 .
Akizungumza baada ya kumshukuru Mbunge kwa kulipia gharama hizo, Spika wa Bunge Mhe Dr. Tulia Ackson kwanza alianza kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji Mkubwa uliokwisha fanyika hospitalini hapo na kwamba yanayoonekana ni matunda ya uwekezaji huo. Pamoja na hayo aliwashukuru wote waliojitolea kusaidia ujenzi huo ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, na viongozi wa Chama kwa niaba wa wote.
Katika msafara huo watu 27 walijeruhiwa ambapo wote wameruhusiwa isipokuwa wawili ambao watabaki chini ya uangalizi na wawili walifariki Dunia kwa majeraha waliyoyapata katika ajali hiyo.
0 Comments