Na Omar Mbarak
Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anazungumza na watumishi wa Halmashauri ya Chalinze katika Ukumbi wa Mikutano wilayani hapo.
Mhe. Kikwete alitumia mkutano huo kuwakumbusha watumishi umuhimu wa kufanya kazi kuzingatia misingi ya kazi ikiwemo kujitambua na kutambua tunaowahudumia. Katika kusistiza utumishi wenye tija na weledi, Mhe Naibu Waziri aliwakumbusha watumishi kuendelea kuwahudumia wananchi wote sawa na hakuna sababu ya kuchagua na kuweka madaraja katika utoaji wa huduma.
Katika mkutano huo , Mhe. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha umuhimu wa kutochagua vituo vya kazi huku akiwakumbusha kuwa uchaguzi wa Vituo vya kazi unalenga sio tu kuwasaidia baadhi lakini unatengeneza madaraja katika utumishi wa umma. Hivyo Mhe. Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwaasa watumishi wa umma kutochagua vituo vyq kazi. Popote ambapo utapelekwa pana hadhi ya mtumishi kufanya kazi na kuwakumbusha hasa wazazi kuacha utaratibu wa kupiga simu za kuwaombea watoto wao vibali vya kuhamishwa vituo wapelekwe mijini.
Katika kikao hicho Mhe Kikwete pia aliwapongeza watumishi wa halmashauri hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya.
0 Comments