Kata ya Kibindu, Chalinze
Katika Muendelezo wa Ziara ya Mh. Mbunge Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, leo ilikuwa zamu ya Kata ya Kibindu. Akiwa katika kata ya Kibindu , Mbunge huyo wa Jimbo amekagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya Elimu, Maji, TASAF,Ujenzi wa miundo Mbinu ya Barabara, kupokea taarifa za maendeleo ya kituo Cha Afya na Zahanati na kuongea na wananchi katika vijiji vya Kwa Mduma na Kibindu.
Akiwa katika kijiji cha Kwa Mduma , Mbunge amewahakikishia wananchi kuwa mradi wa maji toka Mjembe utakwisha na wananchi watafikishiwa maji ndani ya muda. Kuhusu ujenzi wa madarasa, Mbunge ameishukuru serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu kwa madarasa na ongezeko la Walimu jambo pia linaenda sanjari na ongezeko la watoa huduma wa afya.
Akiwa Kibindu, Mbunge amewatoa wasiwasi wananchi kuwa serikali yao itakamilisha ujenzi wa miundo mbinu ya barabara na mashule ndani ya Muda. Pia , amewapongeza wananchi kwa kumuunga mkono Diwani wao Ndg. Mkufya Mawazo ambaye pia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Chalinze.
0 Comments