Blog Post

MHE UMMY MWALIMU MBUNGE WA TANGA AWAPONGEZA BOTNAR FOUNDATION

 MBUNGE UMMY  MWALIMU ATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA  NA BOTNAR FOUNDATION


Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 17/07/2023 ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na  Botnar Foundation awamu ya kwanza ambapo kwanza aliwashukuru kwa kukubali ombi lake la kuja Jiji la Tanga kutekeleza miradi ya kuwainua wananchi wa   Jiji la Tanga. Jumla ya fedha zilizotumika hadi sasa ni kiasi cha shilingi bilioni 5.65 zimetumika.


Miradi hiyo ni ya uvuvi, kilimo cha mwani, jongoo bahari na unenepeshaji wa kaa pamoja na ufugaji wa samaki, kuku na kilimo cha mbogamboga katika kata za Tongoni, masiwani, Tangasisi, Usagara na Central. Aidha Botnar foundation pia wamefadhili miradi ya Afya, Elimu na kujenga Forodhani ya Tanga.


Mhe mbunge amewashukuru Botnar foundation kwa msaada huo na kuwaomba kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo kwa awamu nyingine ili kuchochea maendelea ya Tanga Mjini na wanaTanga.


Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda amemuhakikishia Mhe Ummy kuwa Botnar itaendelea kushirikiana nae na Halmashauri ya Jiji la Tanga katika kutatua kero za maendeleo kwa wakazi wa Tanga Mjini hususan vijana na watoto.


Katika ziara hiyo mhe mbunge aliongozana na sekretariet ya ccm wilaya ikiongozwa na Katibu wa CCM ndugu Selemani Sankwa, madiwani wa kata zenye miradi na wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.


Imetolewa na;-

Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini

17/07/2023

Post a Comment

0 Comments

Close Menu