Na Mwandishi wetu Kahama Shinyanga
Afungua rasmi maonesho ya SIDO kwa mwaka 2026 Wilayani Kahama.
Asisitiza umuhimu wa kuchakata malighafi kuongeza thamani badala ya kuuza bidhaa ghafi.
Serikali ya awamu ya Sita kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya mikopo kwa Wajasiriamali.
Aagiza Kongani za Viwanda kuanzishwa Wilaya zote nchi nzima.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga (Mb) amelitaka Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo[ SIDO kuongeza juhudi katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kupata teknolojia na mashine za gharama nafuu zitakazowawezesha kuongeza thamani ya malighafi,kukuza biashara na kutengeneza ajira nchini.
Mhe.Kapinga ameyasema hayo, jana Oktoba 24,2026 Wilayani Kahama Mkoani wa Shinyanga ,wakati wa ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa 2026 ambapo amesema Tanzania ina utajiri wa rasilimali zinazotokana na Kilimo,Mifugo,Uvuvi,Misitu na nyinginezo ambazo zinaweza kutumika kama msingi wa kuendeleza Viwanda na Biashara zenye tija na kusisitiza umuhimu wa kuchakata malighafi nchini ili kuongeza thamani badala ya kuuza bidhaa ghafi.









0 Comments