Blog Post

RAIS DKT MWINYI KUELEKEA KOREA KUSINI KUSHIRIKI MAJUKWAA YA UTALII


Na Omar Mbaraka


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuondoka nchini leo, tarehe 25 Oktoba 2026, kuelekea Korea Kusini kushiriki Jukwaa la 27 la Sera za Utalii kwa Visiwa na kutembelea Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026, yatakayofanyika Jijini Yeosu, katika Kisiwa cha Jeju.


Ushiriki huo unalenga kuitangaza Zanzibar kimataifa, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii, kuvutia uwekezaji na kuongeza idadi ya watalii, hatua zitakazochangia kukuza uchumi na fursa za ajira kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu