Blog Post

HALE CUP 2026 YAANZA KWA KISHINDO HUKU BANYAMULENGE YAICHAPA WATUMISHI 6 KWA 1









 Na Mwandishi wetu Hale Korogwe Tanga


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Zytun Swai, leo Oktoba 20, 2026, amefungua rasmi mashindano ya Hale Cup 2026, yanayodhaminiwa na Taasisi ya Dkt. Abbasi Foundation kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya vijana katika michezo.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Swai amesema mashindano hayo yana mchango mkubwa katika kutambua na kukuza vipaji vya vijana, huku akitoa shukrani kwa Taasisi ya Dkt. Abbasi Foundation kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.


Aidha, ameiomba taasisi hiyo kuanzisha mashindano ya Hale Cup kwa upande wa wanawake ili kutoa fursa zaidi kwa wanawake kuibua na kukuza vipaji vyao vya michezo.


Ufunguzi wa mashindano hayo umepambwa na mchezo wa soka kati ya Timu ya Watumishi na Timu ya Banyamulenge, ambapo Banyamulenge imeibuka na ushindi wa mabao 6-1.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dkt. Abbasi Foundation, Dkt. Hassan Abbasi, amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuibua vipaji vya vijana na kuwawezesha kupata fursa ya kucheza katika timu kubwa za ligi.


Mashindano ya Hale Cup 2026 yanatarajiwa kuhitimishwa Januari 1, 2027.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu