Blog Post

MVUA YENYE UPEPO MKALI YATIKISA RORYA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO MMOJA DC MHE MABULA ATOA POLE





Na Mwandishi wetu

Mvua iliyoambatana na upepo mkali ilidumu kwa takribani dakika thelasini Alfajili ya Tarehe 08.10.2026 na kusababisha kifo cha mtoto wa miaka mitatu pamoja na madhara ya binadamu ikiwemo ubomoaji nyumba na uezuaji wa mapaa kwa baadhi nyumba 14 katika Wilaya ya Rorya, Tarafa ya Suba.


Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Stanslaus Mabula akiwa ameambatana na kamati ya usalama wamefika katika Kijiji cha Isango katika Kata ya Nyabuga na kutoa pole kwa famili zilizopata madhara kutokana na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali. DC Mabula amewasihi wakazi wa Wilaya hiyo kuchukua tahadhari ya mvua ya EL-Nino na kuelekeza wahanga waliopata majeraha wa tukio hilo kupata matibabu bure.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu