Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Judith Kapinga amesema katika kipindi cha mwaka 2025/2026 jumla ya viwanda vipya vikubwa na vya kati 25 vimejengwa na kuanza uzalishaji nchini.
Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara Bungeni jijini Dodoma leo Mei 22, 2026, Waziri Kapinga amesema viwanda hivyo vimejengwa katika sekta mbalimbali ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha mazingira ya biashara na kukuza uchumi wa viwanda.
Aidha, amesema viwanda hivyo vimetoa jumla ya ajira 39,250 ambapo ajira za moja kwa moja ni 7,635 huku ajira zisizo za moja kwa moja zikiwa 31,615.
Serikali imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya malighafi za ndani, kuongeza uzalishaji wa bidhaa pamoja na kukuza mauzo ya bidhaa nje ya nchi.




0 Comments