Na Mwandishi wetu Arusha
Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Balozi Dr. Emanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania umewakutanisha Wana-TAPSEA takriban 5050 toka Serikali zote na Halmashauri zote pamoja na taasisi mbalimbali toka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Akizungumza katika mkutano huo Makamu wa Rais, Mhe Dr. Nchimbi amewahimiza wajumbe wa mkutano huo ambao utakamilika kwa kuchagua uongozi mpya wa Chama Chao kuzingatia haki na kwamba waepuke masuala yote yatakayo kipotezea muelekeo chama chao.
Nae Mhe Kikwete akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, aliwakumbusha wanataasisi hao juu ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha kuwa wafanyakazi nchini wananeemeka na matunda ya serikali yao kwa kuwakumbusha kuwa serikali imepandisha madaraja ya watumishi, imebadili muundo na vyeo, imelipa madeni ya mishahara nk. Na pia serikali inaahidi kuendelea kufanya hivyo katika bajeti hii ya mwaka na kuendelea kila panapopatikana bajeti.






0 Comments