Blog Post

DKT MWIGULU AFUNGUA SOKO LA MAZAO KIBAKWE DODOMA


 Na Mwandishi wetu 


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumamosi (Mei 9, 2026) ameweka jiwe la msingi la ufunguzi wa soko la mazao Kibakwe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma.


Ujenzi wa soko hilo umelenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kupata maeneo rasmi, salama na yenye miundombinu stahiki kwa ajili ya biashara ya mazao yao.


Akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa soko hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitambulisha kuwa kiongozi wa matokeo kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania


“Mheshimiwa Dkt. Samia ni  mtendaji. Ambaye akisema jambo, anatekeleza. Na haya yanadhihirishwa kwa kazi kubwa ambayo imefanyika”


Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya kazi kubwa inayowapa heshima Watanzania wote. “Nchi inapopiga hatua, kwa kazi kubwa inayofanywa Rais wetu, inalinda heshima ya uhuru wa nchi”.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu