Blog Post

WIZARA YA NISHATI YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO DODOMA







 Na Mwandishi wetu 

Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo  ambayo  yameanza Tarehe 1  Agosti Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma.

Maonyesho hayo yamebebwa na kaulimbiu iya " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025", 

Katika maonyesho hayo ambayo yamefunguliwa na   Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor  Mpango, Watalaam wa Wizara pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Nishati ikiwemo ukamilishaji wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na Usambazaji wa Umeme Vijijini, wanatoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia 

Aidha wananchi wanafahamishwa kuhusu mipango mbalimbali ambayo Wizara imepanga kutekeleza katika mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kusambaza umeme vitongojini na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Taasisi za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maonyesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA),  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)  Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania ( TGDC).

Post a Comment

0 Comments

Close Menu