Na Mwandishi wetu
Umoja wa vikosi hai vya Comoro dhidi ya serikali (FCFVC) vinadai bw Bashar aliekamatwa jijini Dar es salaam nakupelekwa Comoro ambapo anashikiliwa aachiwe huru
Bw Abdoussalam Ibrahim anaejulikana kwa jina la Bashar anadaiwa kuwa ni mwanaharakati anaepinga siasa za RAIS wa Comoro Azali Assoumani
Bw Bashar ambae anadai kuwa RAIS wa Sasa anapotosha uhuru na haki na hivyo kuendesha nchi bila kufuata Sheria kwani wanasiasa wengi wamewekwa ndani kwa kusema ukweli
Kwa mujibu wa 'press release' iliosambazwa tarehe 12 may 2025katika vyombo vya habari kutoka makao makuu ya FCFVC ufaransa inasemekana bw Bashar aliwekewa mtego wa rushwa na ubalozi wa Comoro na hatimae kukamatwa Alhamisi ya tarehe 8 may 2025 na kupelekwa Comoro jumamosi ya tarehe 10 may 2025
FCFVC inadai maisha ya bw Bashar yapo mashakani na wala hatafikishwa katika vyombo vya sheria pia wanasema Hali ya maisha kwa ujumla si shwari Kuna uongozi wa mabavu hivyo wanaomba Dunia kufatilia wakiwemo umoja wa Afrika,SADC,umoja wa mataifa ,mashirika ya kimataifa ya haki za kibinadamu na serikali rafiki kama Tanzania.
0 Comments