Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete amefanya kikao kazi na viongozi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma, Abdulrahman Mohamed Msham, Taasisi ya OSHA wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda pamoja na viongozi wa Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross Society ).
Kikao hicho kimefanyika tarehe 12 Mei 2025 jijini Dodoma.
Katika kikao hicho kwa pamoja wamejadili na kuelekeza kuimarisha mashirikiano ya kazi katika kipindi cha majanga. Pia Mhe Kikwete amewapongeza kwa utayari wa viongozi wa pande zote kuhakikisha maslahi ya Wananchi yanakuwa ya kipaumbele.
0 Comments