Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) mnamo Tarehe 10, Mei 2025, ameshiriki uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Uwanja wa Azimio Mtende Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika uzinduzi huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na kuhudhuliwa na Viongozi Mbalimbali wa Serikali, wadau wa sheria ina dhima ya kutoa wigo mpana kŵa wananchi kupata elimu na msaada wa jisheria dhidi ya Masuala ya Mirathi, Migogoro ya Ardhi, Ndoa, Madai pamoja na Masuala ya unyanyasaji na uharifu wa haki za binadamu ikiwemo ukatili wa Kijinsia.
MCC Chatanda amesema, kila mwananchi ana haki ya kupata usaidizi wa Kisheria pale anapohitaji na Wahanga wakubwanawake kwa kuwa hupoteza haki zao za Msingi na kuishia kulalamika, hivyo serikali kuja na huduma hiyo ya utoaji wa Msaada wa Kisheria bure Itawasaidia Watanzania walio wengi hususani wanawake.
0 Comments