Blog Post

WAZIRI KIKWETE AHUDHURIA UZINDUZI WA BODI YA WADHAMINI YA PSSSF

 Na Omary Mbaraka 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki sherehe za uzinduzi wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Machi 27, 2025, jijini Dar es Salaam.


Katika Shughuli hiyo , pamoja na mengineyo naliitaka Bodi hiyo kuhakikisha inasimamia uwekezaji wenye tija wa Mfuko huo na mipango ya kutoa huduma bora kwa wanachama uku ikiendeleza matumizi ya TEHAMA ili kuwarahisishia wanachama wake kupata huduma kirahisi kupitia simu zao na njia ya kompyuta kwa wale wenye ukaribu na njia hizo.


Aliwatakia kheri pia katika kutekeleza majukumu na msisitizo akauweka katika kutimiza majukumu yao na kuepuka migongano isiyo ya lazima na Menejiment katika kutekeleza majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu