Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, amekabidhi zawadi za Sikukuu ya Iddi katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto mkoani humo, zawadi zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwasilisha salamu za Mhe. Rais, Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa Dkt. Samia ametoa zawadi hizo ili kuhakikisha watoto hao wanafurahia sikukuu wakiwa na mahitaji ya msingi, ikiwemo chakula.
Aidha, Balozi Dkt. Batilda amewapongeza walezi wa watoto hao kwa malezi bora yenye misingi ya maadili, huku wakiendeleza vipaji vyao.
Kwa upande wao, walezi wameeleza shukrani zao kwa Rais Dkt. Samia kwa kuwakumbuka watoto hao, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu, jambo ambalo limewapa faraja na kuondoa upweke.
Nao watoto kutoka vituo mbalimbali wamemuombea dua Mhe. Rais Samia, wakimtakia afya njema na uongozi wenye mafanikio.
0 Comments