Blog Post

SERIKALI YATOA NAFASI 8000 ZA MAFUNZO KWA VIJANA

 


Na Omary Mbaraka 

Ofisi ya waziri mkuu wizara ya kazi, ajira,vijana na wenye ulemavu kitengo Cha mawasiliano ya serikali,imetangaza nafasi 8000 za mafunzo mbali mbali kwa vijana wenye miaka kuanzia 15-35 wakati huo huo vijana wenye ulemavu kupewa kipaumbele.

Nafasi hizo ni katika fani zifuatazo; ufundi wa magari, ufundi umeme wa magari na nyumba, ushonaji nguo, upakaji rangi, udereva wa magari, huduma za hoteli na utalii, ukataji wa madini  upakaji rangi magari nk.

Serikali itagharamia ada kwa asilimia mia moja hivyo basi maombi haya yatapokelewa kuanzia tarehe 30 January 2025 mpaka tarehe 15 February 2025 Maombi haya pia yanapatikana katika tovuti  www,kazi,go,tz 

Waombaji waombe katika chuo kilichopo mkoa anaoishi

Post a Comment

0 Comments

Close Menu