Blog Post

SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO MIAKA 48 YA CCM

 


Na Omary Mbaraka 

𝑨𝒃𝒂𝒊𝒏𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒌𝒖𝒘𝒂 𝑹𝒂𝒕𝒊𝒃𝒂 𝒚𝒂 𝑴𝒂𝒂𝒅𝒉𝒊𝒎𝒊𝒔𝒉𝒐 𝒉𝒂𝒚𝒐 𝒌𝒖𝒕𝒂𝒏𝒈𝒖𝒍𝒊𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝑴𝒃𝒊𝒐 𝒛𝒂 𝑴𝒂𝒓𝒂𝒕𝒉𝒐𝒏 𝒛𝒂 𝑼𝑽𝑪𝑪𝑴 𝒎𝒂𝒑𝒆𝒎𝒂 𝒂𝒔𝒖𝒃𝒖𝒉𝒊 𝒑𝒂𝒎𝒐𝒋𝒂 𝒏𝒂 𝑲𝒐𝒏𝒈𝒂𝒎𝒂𝒏𝒐 𝒍𝒂 𝑼𝑾𝑻 𝒍𝒊𝒕𝒂𝒌𝒂𝒍𝒐𝒇𝒂𝒏𝒚𝒊𝒌𝒂 𝑼𝒌𝒖𝒎𝒃𝒊 𝒘𝒂 𝑱𝑲𝑪𝑪 - 𝑫𝒐𝒅𝒐𝒎𝒂 𝒕𝒂𝒓𝒆𝒉𝒆 4 𝑭𝒆𝒃𝒓𝒖𝒂𝒓𝒊, 2025

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla ametoa tamko la CCM ya kuwa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM yatafanyika Jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri tarehe 5 Februari, 2025.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kutokea Kisiwani Zanzibar leo tarehe 1 Februari, 2025, CPA. Malkalla amebainisha kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo kitaifa  anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025 𝐍𝐝𝐮𝐠𝐮. 𝐒𝐚𝐦𝐢𝐚 𝐒𝐮𝐥𝐮𝐡𝐮 𝐇𝐚𝐬𝐬𝐚𝐧.

CPA. Makalla ameeleza kuwa CCM inaenda kuadhimisha miaka 48 ikiwa bado Chama cha Siasa Imara chenye kuendelea kushika dola na kutekeleza Ilani yake kwa vitendo jambo ambalo limeendelea kuwapa imani kubwa ya kuaminiwa zaidi na Wananchi.

"𝑪𝑪𝑴 𝒊𝒏𝒂𝒕𝒊𝒎𝒊𝒛𝒂 𝒎𝒊𝒂𝒌𝒂 48 𝒏𝒂 𝒋𝒂𝒎𝒃𝒐 𝒌𝒖𝒃𝒘𝒂 𝒏𝒊 𝒌𝒘𝒂𝒎𝒃𝒂 𝑪𝑪𝑴 𝒏𝒅𝒊𝒚𝒐 𝒊𝒍𝒊𝒚𝒐𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒓𝒊𝒅𝒉𝒂𝒂 𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒖𝒏𝒅𝒂 𝒔𝒆𝒓𝒊𝒌𝒂𝒍𝒊, 𝒏𝒅𝒊𝒚𝒐 𝒚𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒊𝒍𝒂𝒏𝒊 𝒏𝒂 𝒊𝒏𝒂𝒕𝒆𝒌𝒆𝒍𝒆𝒛𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒗𝒊𝒕𝒆𝒏𝒅𝒐 𝒉𝒊𝒗𝒚𝒐 𝒕𝒖𝒏𝒂𝒂𝒅𝒉𝒊𝒎𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒎𝒊𝒂𝒌𝒂 48 𝒕𝒖𝒌𝒊𝒘𝒂 𝒄𝒉𝒂𝒎𝒂 𝒊𝒎𝒂𝒓𝒂 𝒄𝒉𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒔𝒆𝒓𝒊𝒌𝒂𝒍𝒊 𝒊𝒎𝒂𝒓𝒂 𝒏𝒂 𝒄𝒉𝒂𝒎𝒂 𝒂𝒎𝒃𝒂𝒄𝒉𝒐 𝒌𝒊𝒎𝒆𝒆𝒏𝒅𝒆𝒍𝒆𝒂 𝒌𝒖𝒂𝒎𝒊𝒏𝒊𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒘𝒂𝒏𝒂𝒏𝒄𝒉𝒊"

Aidha, CPA. Makalla amesema kuwa sherehe za shamrashamra zimeanzia katika mikoa mbalimbali tangu tarehe 28 Januari, 2025.



Post a Comment

0 Comments

Close Menu