Blog Post

DKT HENJEWELE AWAASA WAPIGA PICHA KUJISAJILI ILI PIA WAWEZE KUPATA MKOPO

 Na Omary Mbaraka 


Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania (SHISAMA) Dkt. Cynthia Mwambeleko Henjewele, ameshiriki akiwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu Chama cha wapiga picha wa kwenye Sherehe Tanzania,  uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho jiji Dar es Salaam.


Dkt. Henjewele aliwapongeza kwa Mkutano huo Wapiga picha hao wa Sherehe mbalimbali, kwenye hotuba yake asisitiza waendelee kujisajili kwenye vyama na mashirikisho ili waweza kutambulika rasmi na kuweza kupata faida mbalimbali ikiwa pamoja na Mikopo ya Wasanii iliyotolewa na Mh Daktari  Msma Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa Wasanii nchini.


Pia aliwapongeza kwa kuwa pamoja na kuona Sanaa ya upigaji picha ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na kuweza kuwaingizia kipato kwao na Serikali.


Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Bw Rajab Mchatta  alikabidhiwa kitabu cha Muongozo wa Maadili ya Msanii kilicho tolewa na Taasisi Basata iliyo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo.


Aidha, Dkt. Henjewele alisisitiza wapiga picha hao wa picha za Mnato na  picha Jongefu hasa wa kwenye Sherehe wafwate sana maadili kwa kutopiga picha zisizofaa na kurusha kwenye mitandao ya kijamii kwani inaharibu maadili ya Mtanzania, aliwatakia kila la kheri kwa mwaka huu na kuwahimiza kuendelea kufanya Mkutano huo Mkuu kila mwaka



Post a Comment

0 Comments

Close Menu