Na Omary Mbaraka
Stephen Masato Wasira, amepitishwa kwa kishindo na mkutano mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alipata kura 1917 kati ya kura 1924.
Katika maelezo yake mafupi aliyoyatoa mara baada ya kuchaguliwa na kushangiliwa na umati mkubwa alisema "Kazi iliopo mbele yetu ni kushinda katika uchaguzi mkuu kwani serikali chini ya CCM imefanya mambo makubwa ikiwa kuwatimizia wananchi mahitaji yote ya msingi kama vile kujenga mahospitali nchini kote, Shule za kutosheleza, kujenga barabara kote nchini zikiwemo "flyover na mahitaji yote muhimu, ikiwa pia kukamilisha bwawa la mwalimu nyerere pamoja pia kuwatua waakinamama ndoo. kichwani, kujenga reli ya SGR, Daraja la magufuli la busisi hivyo haoni kwa nini washindwe
Mhe Wasira alisema ni wakati wa kuendeleza fikra za Raisi wetu Mhe dkt Samia Suluhu Hassan za kufanya maridhiano kwa jamii yote wakiwemo watu wa nchi za nje,mabalozi na wananchi
Hivyo basi aliwakumbusha wanachama wa CCM kuwa ibara ya Tano inasema kukamata dola ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar na Sasa anaanza kazi hio
Nae Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan alisema "Mapema leo, nimeungana na wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum hapa mkoani Dodoma."
"Pamoja na mambo mengine, mkutano huu umemchagua Ndugu Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ninampongeza sana, na ni dhahiri kuwa atakuwa na mchango wa kipekee katika kuimarisha utendaji wa chama chetu." Mama Samia aliongeza
"Kupitia mkutano huu pia tumepokea na kujadili utekelezaji wa kazi za Chama na Jumuiya zake kwa kipindi cha miaka miwili (2022-2024). Tumesikia juu ya kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, na tumeazimia kuwafikia Watanzania wengi zaidi katika maeneo yao, na kutatua changamoto zao katika safari ya kufurahia matunda ya uhuru wetu."Alinena Mama Samia
Katika mkutano huo mkuu alihudhuria pia Raisi mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pia Raisi mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume pia katibu mkuu mstaafu Abdulrahamani Kinana na mawaziri wakuu wastaafu
0 Comments