Na Ismail Mang'ola
UJENZI wa jengo la ofisi ya Serikali ya mtaa wa Chang'ombe 'B' Kata ya Chang'ombe Manispaa ya Temeke inayojengwa kwa nguvu ya wananchi umekwama.
Ujenzi huo ambao ulianza kwa kasi baada ya wananchi wa mtaa huo kufahamishwa kuhusu nyumba ilivyokuwa ofisi hiyo imepangwa kuuzwa, wananchi walijitolea kuchangia ujenzi wa hiyo nyumba lakini kwa Sasa umekwama kutokana na nguvu ya wananchi kuishia hapo.
Akitoa ufafanuzi katika mkutano wa maendeleo ya mtaa huo ambao hufanyika Kila baada ya miezi mitatu, mwenyekiti wa mtaa wa Chang'ombe 'B' Ally Said Majata alisema kuwa, kiasi kinachohitajika kumalizika ujenzi huo ni T sh 5,000,000 za kitanzania ambazo NI kwa ajili ya mabati, mbao, misumari, GYPSUM pamoja na malipo ya mafundi.
Majata aliendelea kuwaeleza wananchi kuwa, jengo la ofisi linajengwa katika eneo la wazi la uwanja wa michezo wa Mabembeani sambamba na shule ya Sekondari ya Kata ya Chang'ombe ambayo ujenzi wake unatarajia kuanza siku sio nyingi Hali ambayo itawapunguzia wanafunzi hao umbali wa kufuata masoma ambako kwa Sasa wanasoma katika shule ya Sekondari Keko Magurumbasi.
Aidha Majata amewataka wazazi kuhakikisha wanawasimamia vyema watoto katika jukumu la ulinzi kwa mtoto hasa katika kuhakikisha Usalama wao wakati wa kurudi nyumbani hasa kutokana na matukio ambayo yamekuwa changamoto kwa watoto wetu sambamba na kutekwa.
Akizungumzia kuhusu suala la ulinzi na Usalama katika mtaa wa Chang'ombe 'B' amewataka wananchi kutowakimbia wakusanyaji wa michango ya ulinzi shirikishi ambapo wengi' wao wamekuwa wakiwakimbia wakusanyaji hao Huku wengine wakikaidi kwa maksudi.
Amewataka wale wote wanaokaidi kulipa michango ya ulinzi shirikishi na kusema wote watachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu jukumu la ulinzi na Usalama lipo juu ya wananchi kujilinda wenyewe, alisema Chaimeni Majata.
Pia akizungumzia kuhusu usafi wa mazingira Majata alisema, hakuna mtu ambaye anaweza kutoka Kinondoni ama Gongolamboto aje afanye usafi kwenye eneo lako, hivyo jukumu la usafi wa mazingira ni wa Kila mkazi na afanye usafi katika eneo la makazi yake.
0 Comments