Blog Post

KOMRED KITTE AONGOZA JESHI LA MAMA SAMIA KUFUNGUA KAMPENI KIBAHA MJINI

 Na Omary Mbaraka 


Tarehe 21/11/2024, Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, *Ndugu Kitte Mfilinge,* ameongoza mamia ya wanachama wa CCM, wananchi na wapenda maendeleo katika ufunguzi rasmi wa kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Wilaya ya Kibaha Mjini.


Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya kwambonde, Ndugu Kitte, aliye kuwa mgeni rasmi, alisisitiza kuwa lengo kuu la CCM ni kushinda uchaguzi huu, kutokana na Mambo makubwa Miradi ya Maendeleo iliyofanywa katika Wilaya ya Kibaha na serikali yetu ya CCM chini ya  *Dkt Samia Suluhu Hassan*. 


_*"CCM ni chama chenye nguvu na uwezo wa kushinda na Tuna uzoefu mkubwa katika kusimamia maendeleo, na ni chama pekee kilichowezesha mafanikio makubwa kwa wananchi,"*_ alisema Ndugu Kitte.

Aidha Mheshimiwa Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, aliongeza kuwa _ *CCM imetekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa mafanikio makubwa, hasa katika miradi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi._* "Hatutegemei kushindwa kwa sababu utekelezaji wa Ilani yetu ya uchaguzi tumekuwa na matokeo chanya kwa wananchi wa Kibaha na miji mingine nchini," alisema Mheshimiwa Koka, akiwahakikishia wananchi kuwa CCM inatoa huduma bora katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na usalama.


Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Nyamka, alielezea hari na hamasa kubwa ya wanachama wa CCM katika wilaya hiyo, akithibitisha kuwa CCM Kibaha Mjini iko tayari kwa mapambano ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na lengo ni kuhakikisha ushindi katika mitaa yote 73 ya wilaya. "Huu ni wakati wa kushirikiana na wananchi ili tufikie malengo yetu. Tumejipanga vema kwa ushindi wa heshima kwa ajili ya Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye anahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote," alisisitiza Mwl. Nyamka.


Uzinduzi wa kampeni hizo umehudhuriwa na mamia ya wanachama, viongozi wa serikali, na wananchi wa Wilaya ya Kibaha Mjini, na umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuonyesha mshikamano na utayari wa CCM kushinda katika uchaguzi ujao.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu