Blog Post

BODI ZA USAJILI WA WAKANDARASI (CRB) NAUHANDISI(ERB) ZAPUUZWA




Na Ismail Mang'ola, Dar


Kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa nne Kariakoo jijini Dar es Salaam, wataalam wanaosimamia na kutoa vibali kwa wakandarasi kwa maana ya CRB, ERB na EQRB Kama wangekuwa wakifatilia na kuzingatia habari zinazoandikwa na mtandao was Kijamii TAFAKARI NEWS WEBLOG, inawezekana maafa haya yasingetokea.


Mtandao wa TAFAKARI NEWS WEBLOG umekuwa ukiripoti aina hii ya ujenzi wa majengo ya ghorofa bila kufuata utaratibu wa kusajili miradi kutokana na wakandarasi wengi' hawana vibali pamoja na vigezo.ama wamiliki kukwepa gharama za vibali ikiwemo Kodi ya serikali


Ama Majengo hayo yasiyokuwa na ubora yamekuwa yakijengwa mitaani hasa maeneo ya vichochoroni wakisingizia kuwa maeneo hayo ni SQUATER kwa maana hayajapimwa Huku wakikingiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za mtaa.


Jengo linguine ambalo linajengwa bila kufuata taratibu lipo Tabata Kinyerezi kwa Makofia linalomilikiwa na bwana mmoja aliyetambulika kwa jina la Simba Mzee, halikusajiliw  kutoka CRB Wala ERB.



Mbali na mapungufu hayo ya ubora wa majengo, pia bado Kuna mapungufu mengi katika saiti hizo Kama vile wafanyakazi hufanya kazi bila kupatiwa vitendea kazi Kama vile' KOFIA NGUMU, VIATU, GLOVE, MKANDA wakati wa kufunga bimu juu pamona na vitendea kazi vingine vinavyohusiana na shughuli za ujenzi.

Hata hivyo tunatoka pongezi nyingi kwa Rais wetu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekeza jeshi la polisi kumhoji mmiliki pia pongezi nyingi ziende kwa waziri mkuu Mhe Majsliwa kwa kushiriki kikamilifu katika sakata hili ikiwa ni pamoja na kuaga marehemu wahanga WA jengo hilo mnazi mmojja

Hivyo basi chombo hiki Cha habari kinaendelea na uchunguzi na kubaini MAJENGO yanayojengwa bila kusajiliwa kuyafichua Ili wahusika wachukue hatua stahiki kuepusha majanga haya

Post a Comment

0 Comments

Close Menu