Na Omary Mbaraka
Serikali itaendelea kuboresha bajeti ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA), Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kutegemeana na hali ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili kuimarisha shughuli za ulinzi na kuboresha miundombinu ya utalii.
Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Esther Edwin Malleko (Mb) aliyetaka kujua kuna mkakati gani wa kuwaongezea bajeti TANAPA na TAWA kwani majukumu yao ni makubwa ikilinganishwa na bajeti inayotengwa.
"Je, kuna mkakati gani wa kuwaongezea bajeti TANAPA na TAWA kwani majukumu yao ni makubwa ikilinganishwa na bajeti inayotengwa?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro aliuliza
"Sekta ya Utalii imekuwa sana hasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutengeneza Filamu ya Royal Tour. Je, Serikali haioni umuhimu wa kurejesha utaratibu wa zamani" aliuliza Mhe Esther Malleko
0 Comments