Na Omary Mbaraka
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani, Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Pwani Cde. Mwinshehe Mlao wakiwanadi wagombea CCM Kata ya Bwilingu jimboni humo.
Kikwete ambaye ni Waziri wa Nchi wa Ajira Kazi na Vijana Wenye Ulemavu, pia aliendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha chama hicho kwa kuzindua mashina mapya Manne (4) ya wanachama wakereketwa katika kitongoji cha Bwilingu.
Mhe Kikwete amesema Mapokezi ya Wananchi yanatoaishara kuwa CCM itashinda kwa asilimia kubwa sana uchaguzi wa serikali ya mtaa unaofanyika nchini nzima mwaka huu.
Zifuatazo ni picha zinazoonyesha matukio mbalimbali ya zoezi la kuwanadi wagombea wa chama hicho kata Bwilingu.
0 Comments