Blog Post

MHE RIDHWANI KIKWETE AWAHAKIKISHIA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NA VIJANA KUWA SERIKALI ITAWASAIDIA

 

 Na Omary Mbaraka 

Waziri WA nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,ajira na vijana wenye ulemavu Mhe Ridhwani Kikwete awahakikishia Wajasiriamali Wanawake na Vijana kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha Wajasiliamali kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili waweze kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii kwa ujumla. Serikali inaamini ukisaidia makundi haya muhimu umesaidia Jamii. 


Kauli hiyo aliitoa  kwenye uzinduzi wa Jukwaa la soko la Bidhaa zinalnazozalishwa na wajasiliamali Wazawa Wasichana na Vijana la Panda linaloratibiwa na Taasisi ya Her Initiatives linaloongoza na Bi. Lydia Thomas.  Taasisi hii inajulikana kutokana na juhudi kubwa wanazozifanya duniani kuwanyanyua vijana na Wanawake,ambapo wameshinda Zawadi za Utambuzi maeneo mengi ikiwemo ile ya Global Citizen inayotolewa Marekani na ile inayotolewa na Mfalme wa Ubelgiji.




Post a Comment

0 Comments

Close Menu