Blog Post

WATURUKI WATOA MSAADA WA NG'OMBE 1500 WALIOCHINJWA SIKU YA EIDE

*KIKWETE NA WADAU WAWEZESHA KUCHINJWA KWA NG'OMBE ZAIDI YA 1500 NA KITOWEO KUGAWIWA KWA WANANCHI SIKU YA EID.* Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na wadau wake hasa Jumuiya ya Waturuki wameweza kuchinja ng'ombe zaidi ya 1500 na nyama yote kuigawa kwa wananchi mbalimbali ndani ya Jimbo lake la Chalinze kwa ajili ya wananchi kupata kitoweo na kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid Al Adha inayosherekewa na Waislamu kote duniani na maalumu kwa ajili ya kuchinja. Kikwete kwenye mitandao yake ya Kijamii amendika:- "Allah ametujalia kheri katika siku ya leo ya EidAlAdha ambapo tumechinga Ng’ombe zaidi ya 1500 katika maeneo mbalimbali ya halmashauri yetu. Binafsi nikiwa eneo la Kiwangwa ambapo Ng’ombe 800 wamechinjwa tukishirikiana na Jumuiya ya Waturuki na nyama kugaiwa maeneo mbalimbali ya Halmashauri q/s320/IMG-20240620-WA0004.jpg"/>

Post a Comment

0 Comments

Close Menu