Blog Post

MTANZANIA ANUNUA KIWANDA CHA CEMENT KIKUBWA AFRIKA MASHARIKI NCHINI KENYA


Na Omary Mbaraka 

Mtanzania bw Edha Abdallah Nahdi kupitia kampuni ya Amson Group of Companies amenunua kiwanda cha cement nchini Kenya ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vingine vyote vya cement Afrika mashariki Bw Edha ambae ni mkurugenzi mtendaji wa Amson Group of Companies amenunua kiwanda hicho kijulikanacho Bumburi cement kwa T shs milioni 260.

Bumburi cement inazalisha cement ijulikanao Tembo Kiwanda hicho cha Bumburi cement kipo Nairobi na Mombasa na huzalisha wastani wa tani milioni 3.2 kwa mwaka wakati huo huo kiwanda cha mbeya cement

 kinachomilikiwa na kampuni mama ya Amson kinazalisha tani milioni 1.6 na hivyo sasa Amson Group of Companies itazalisha wastani wa tani milioni 4.8 kwa mwaka Kampuni ya Amson Group of Companies inamiliki pia kampuni kongwe ya Camel oil

 inayojishughulisha na kuagiza mafuta ya petroli na Dizeli kutoka nje ya nchi na kusambaza kote nchni na nje ya nchi Malawi Congo Zambia nk Pia kampuni Amson inajishughulisha na uzalishaji wa unga wa ngano nk 

 Chombo hiki cha habari kilipoongea na kiongozi mmoja serikalini ambae hakutaka jina lake kutajwa alisifu juhudi kubwa za bw Edha na kusema ni mfano wakuigwa kwa kupanua wigo huu wa kibiashara kwani kutaongezea pia thamani ya pesa zetu Pia tulizoea kuona wakenya wengi ndio wanakuja kuwekeza hapa nchini

Post a Comment

0 Comments

Close Menu