Blog Post

MSOGA MARATHON KUUNGURUMA JUNI 29 KWENDA KUSAIDIA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Na Omary Mbaraka Hatimaye ni Juni 29, 2024. Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na Viongozi wenzake wa Chalinze wamekuja na MSOGA HALF MARATHON kwa ajili ya kukimbia wakati huo huo kuchangisha fedha ili kwenda kuboresha huduma za Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Wilaya ya Msoga. Kutakua na mbio za aina 3 kwa maana Km 5, Km 10 na Km 21 na lengo ni kuchangisha na kukusanya zaidi ya Milioni 330 ili kwenda kununua vifaa na kuboresha huduma za Afya kwa Mama na Mtoto pale Msoga Hospitali ambayo inahudumia wananchi wengi sana wa Wilaya ya Bagamoyo. Jisajili sasa kwa Tigo kwa kupiga *150*01# kisha nenda namba 5 halafu 6 halafu 1 hatimaye 1 utakuta Msoga Half Marathon utajisajili kwa Tshs 35,000/= ili tukimbie huku tukienda kusaidia kuokoa vifo vya Mama na Mtoto. Kwa LIPA NO: 15840234 (MSOGA HALF MARATHON).

Post a Comment

0 Comments

Close Menu