Blog Post

MPAKA LEO HII WAPALESTINA 34844 WAMEUAWA NA WENGINE 78414 KUJERUHIWA

Na Omary Mbaraka Mpaka kufikia leo hii inakadiriwa wapalestina wapatao elfu thelathini na nne mia nane arobaini na nne (34844)wameuawa na wengine elfu sabini na nane mia nne kumi na nne (78414) wamejeruhiwa na majeshi ya Israel huko Gaza pia inadaiwa kwa masaa ishirini na nne (24) yaliopita wapalestina hamsini na tano wameuawa Na baada ya Israel kuvamia mji wa Rafah njiani kuingia Gaza na kuzuia misaada ye yote kupita inasemekana baada ya siku tatu mahospitali ya Gaza yatasimamisha kutoa huduma ya mstibabu baada ya kukosa mafuta ya kuendesha hodpitali hizo ikiwemo hospitali ya shifa Hata hivyo jumatatu iliopita wahamasi wamekubali kusimamisha vita ili kukaa mezani na wsisraeli ili kusitisha vita ingawaje Rais wa Israel Netanyahu anasema vita viendelee ili kuwamaliza wahamasi wote huko Gaza. Marekani baada ya kuona wahamasi wamekubali kusitisha vita nao wamesimamisha meli kadhaa zilixokuwa zikiwapelekea waisraeli silaha mbalimbali zikiwemo mabomu

Post a Comment

0 Comments

Close Menu