Blog Post

UMAKUTA YAOMBA HALMASHAURI YA TEMEKE KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA MIUNDO MBINU YA STENDI

Na Omar Mbaraka Pamoja na mafanikio makubwa yanayoonekana katika stendi ya mabasi yaendayo kusini mwa Tanzania,inayosimamiwa na asasi ijulikanayo Umoja wa Mabasi yaendayo kusini mwa Tanzania ( UMAKUTA). Mwenyekiti wake kwa niaba ya asasi hio anaiomba halmashauri ya Temeke kushiriki kusaidiana katika kuboresha miundo mbinu ya stendi hio. Akiongea na Tafakari news Weblog kaimu Mwenyekiti wa UMAKUTA bw Kiboko alianza kwa kuelezea mafanikio mengi ya stendi hio ikiwa ni pamoja na utulivu na kuwatendea haki wasafiri wa kusini mwa Tanzania lakini kubwa ameiomba halmashauri ya Temeke chini ya mkurugenzi wake Elly huruma washirikiane na asasi yao kuboresha miundo mbinu ambayo ni chakavu sana Bw Kiboko alisema kwa vile stendi hio inaipatia pia mapato mazuri halmashauri hio ya Temeke hivyo ni wazi kuwa miundo mbinu ikiboreshwa mapato pia yataongezeka katika hamashauri yetu ya Temeke hivyo ni muhimu kwa halmashauri hio kuweka umuhimu wa kuboresha Hivyo basi bw Kiboko ameomba kikao cha pamoja na mkurugenzi wa Temeke Kaimu mwenyekiti huyo bw Kiboko amesema stendi hio ambayo ipo Mbagala rangi tatu pia inachangia fedha nyingi katika serikali kuu kupitia kodi mbalimbali za TRA zikiwemo pia kutoka kwa wafanyabishara Wanao miliki fremu nyingi za biashara katika stendi hio Bw Kiboko ambae ana kaimu nafasi ya mwenyekiti aliefariki wiki hii alisema asasi yao imesajiriwa kisheria hivyo hivi karibuni watafanya mkutano mkuu cha kumthibitisha kuwa mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya UMAKUTA

Post a Comment

0 Comments

Close Menu