Na Omar S Mbaraka
Utafiti unaoendelea kufanywa na chombo hiki cha habari umegundua kuwa maduka mengi makubwa ya kuuza bidhaa kwa jumla yaliopo maeneo ya Mbagala rangi tatu ndio vituo vikubwa vya kihalifu vya kubadili ("Re bagging ")vifungshio kutoka halisi na kuweka vya bandia ili mradi bei iongezeke ama kufanikisha kuuza bidhaa isio na ubora
Ni bidhaa nyingi zinazofanyiwa mchezo mchafu huo lakini zaidi ni sukari na mchele. Maduka hayo ambayo yanamiliki maghala makubwa hubadilisha sukari iliotoka Brazil ambayo iliingizwa hapa ncini kwa msamaha wa kodi uliotolewa na serikali ili kukidhi mapungufu yaliojitokeza ya sukari hapa nchini na kuwekwa katika vifungashio vya sukari kutoka mtibwa na hivyo kuuza kwa bei ya juu
Pia kwa upande wa mchele wafanyabiashara hao huufanyia ukarabati mchele mbovu ikiwa ni pamoja na kuupakaza mafuta ili unukie na kuonekana mchele bora kutoka kyera mbeya na maeneo mengine na hivyo kuuzwa kwa bei ya juu
Hata hivyo tulipoongea na mtoa habari wetu alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakikamatwa lakini wanaachiwa na wanaendelea na shughuli zao jambo ambalo licha ya wananchi kulishwa mchele mbovu pia wanauziwa bidhaa hizo kwa bei ya juu baada ya kubadili vifungashio
0 Comments