Na Omar Mbaraka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Februari 29,2024 kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea saa kumi na moja na nusu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam.
Rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi hapo awali alilazwa London kwa matibabu na baadae kurudishwa hapa nchini na kulazwa katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani ya Mapafu hadi umauti ulipomfika leo Februari 29,2024
Aidha Mhe Rais Dkt Samia kufuatia taarifa ya msiba huu mzito ametangaza siku saba za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti kuanzia kesho
#PumzikakwaamanimzeeMwinyi.
0 Comments